Chanjo ya MMR (Ukambi, Mumps, na Rubella): Unachohitaji Kujua [2021]
Multi-Language
Supporting Files
-
2021/08/06
-
File Language:
Details
-
Alternative Title:MMR Vaccine (Measles, Mumps, Rubella): What You Need to Know [2021] [Swahili] ; Vaccine Information Statement: MMR Vaccine (Measles, Mumps, and Rubella): What You Need to Know [2021]
-
Corporate Authors:
-
Description:VIS au Taarifa ya Habari ya Chanjo ni hati inayozalishwa na CDC, inayowajulisha wapokea chanjo – au wazazi wao au wawakilishi wao wa kisheria – kuhusu faida na hatari za chanjo wanayopokea. Watoa chanjo wote, wa umma au wa kibinafsi, wanahitajika na Sheria ya Kitaifa ya Majeraha ya Chanjo kwa Watoto (NCVIA – 42 U.S.C. § 300aa-26) kutoa VIS inayofaa kwa mgonjwa (au mzazi au mwakilishi wa kisheria) kabla ya kila dozi ya chanjo maalum. VIS inayofaa lazima itolewe kabla ya chanjo na lazima itolewe kabla ya kila dozi katika mfululizo wa dozi nyingi. Lazima itolewe bila kujali umri wa mpokea: https://www.cdc.gov/vaccines/hcp/about-vis/index.html. VIS zimefasiriwa katika lugha karibu 40. Hizi zinaweza kupatikana kwenye tovuti ya mshirika wa CDC, https://www.immunize.org/vis/. Si kila VIS imefasiriwa katika kila lugha.
Kwa nini kupata chanjo?
Chanjo ya MMR inaweza kuzuia surua, matumbwitumbwi, na rubela.
SURUA (M) husababisha homa, kikohozi, mafua, na macho mekundu yenye maji, na mara nyingi hufuatiwa na upele unaofunika mwili wote. Inaweza kusababisha mshtuko (mara nyingi unahusiana na homa), maambukizi ya masikio, kuhara, na nimonia. Kwa nadra, surua inaweza kusababisha uharibifu wa ubongo au kifo.
MATUMBWITUMBWI (M) husababisha homa, maumivu ya kichwa, maumivu ya misuli, uchovu, kukosa hamu ya kula, na uvimbe na maumivu ya tezi za mate chini ya masikio. Inaweza kusababisha uziwi, uvimbe wa ubongo na/au kifuniko cha uti wa mgongo, uvimbe wenye maumivu wa korodani au ovari, na, kwa nadra sana, kifo.
RUBELA (R) husababisha homa, maumivu ya koo, upele, maumivu ya kichwa, na kuwasha kwa macho. Inaweza kusababisha ugonjwa wa viungo kwa hadi nusu ya wanawake wa ujana na watu wazima. Ikiwa mwanamke anapata rubela wakati wa ujauzito, anaweza kupoteza mimba, au mtoto anaweza kuzaliwa na kasoro kubwa za kuzaliwa.
Watu wengi wanaochanjwa kwa chanjo ya MMR watakuwa salama maisha yao yote. Chanjo na viwango vya juu vya uchanjaji vimefanya magonjwa haya kuwa nadra zaidi nchini Marekani.
-
Subjects:
-
Keywords:
-
Series:
-
Subseries:
-
Publisher:
-
Document Type:
-
Funding:
-
Genre:
-
Place as Subject:
-
Rights:Public Domain
-
CIO:
-
Division:
-
Topic:
-
Location:
-
Pages in Document:2 pdf pages
-
Volume:2021
-
Collection(s):
-
Main Document Checksum:urn:sha-512:980734fb149a5cd54b58ebece03f0e9f9b1c93ee6c44342bd5035a44abe6682e46de37465a2d8319dd5de6d6cd7b1e1b50c5987b2c2e636155b6e805ffebd56c
-
Download URL:
-
File Type:
File Language:
ON THIS PAGE
CDC STACKS serves as an archival repository of CDC-published products including
scientific findings,
journal articles, guidelines, recommendations, or other public health information authored or
co-authored by CDC or funded partners.
As a repository, CDC STACKS retains documents in their original published format to ensure public access to scientific information.
As a repository, CDC STACKS retains documents in their original published format to ensure public access to scientific information.
You May Also Like
COLLECTION
Infectious Diseases